Home KILIMO Shamba Darasa kuwanoa wakulima Iringa

Shamba Darasa kuwanoa wakulima Iringa

0 comment 106 views

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Agustino Mahiga ametoa wito kwa wakulima mkoani Iringa kutumia fursa ya uwepo wa kituo cha mafunzo maalum kwa wakulima na wajasiriamali (Shamba Darasa) kuzalisha mazao yenye tija ili kuinua uchumi wao.

Dk. Mahiga amesema hayo baada ya kutembelea kituo cha Shamba Darasa kilichojengwa kwa ushirikiano na ubalozi wa China kwa lengo la kuwajengea uwezo wafugaji, wakulima pamoja na wajasiriamali wadogo. Waziri huyo amewataka wadau wa sekta hiyo kujitokeza kwa wingi mafunzo yatakapoanza kwani wataaalamu kutoka nchini China kwa kushirikiana na wataalamu wengine kutoka hapa nchini watakuepo na mafunzo yatatolewa bila malipo yoyote.

“Tumeona kuna tatizo katika kilimo, mifugo na elimu, hawa wataalamu watakuja watafanya kama shamba darasa wanakijiji watakuja kushiriki, na kwakuwa wananchi wetu ni wakulima basi wataanza na kilimo tangu hatua za awali na baadae mifugo, nyuki na mengineyo”. Ameeleza Dk. Mahiga.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah amesema uwepo wa shamba hilo utaleta mabadiliko makubwa kwa vijana na ni mbinu mojawapo ya wao kujikomboa kupitia sekta ya kilimo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter