Home VIWANDAUZALISHAJI Bilioni 10 kuinua wabunifu

Bilioni 10 kuinua wabunifu

0 comment 23 views

Wabunifu wakiwemo wajasiriamali na wakulima wanatarajia kunufaika kupitia Mpango wa Chakula Duniani (WFP) uliopo chini ya Umoja wa Mataifa ukishirikiana na Mpango wa Changamoto za Millenium pamoja na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na Ukimwi (MCC) kwa ajili ya kuwawezesha wakulima na wajasiriamali wadogo kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Michael Dunford amesema mradi huo unatarajia kuchukua miaka minne na umetengewa kiasi cha Dola za Marekani 4.5 milioni (Sh.10 bilioni za kitanzania), huku washindi wakiahidiwa kusimamiwa ili kutimiza ndoto zao kupitia miradi waliyobuni.

Mkurugenzi huyo amedai kuwa wazo la kutafuta wabunifu na kuwawezesha ni njia mojawapo ya kusaidia wabunifu hao kufikia ndoto zao pamoja na kuongeza uzalishaji wa chakula salama na chenye kujitosheleza.

“Tumekuwa tukijiuliza namna tutakavyohamasisha wabunifu nchini. Kwa hiyo tulizindua mradi huu Julai 20 lengo likiwa ni kuona kama wapo watanzania wanaweza kuongeza uzalishaji wa chakula na lishe ili kuhakikisha usalama wa chakula”. Amesema Dunford

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter