Home VIWANDA Wananchi washauriwa kujitokeza kwa wingi maonyesho ya SIDO

Wananchi washauriwa kujitokeza kwa wingi maonyesho ya SIDO

0 comment 81 views

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amewataka wananchi mkoani humo pamoja na maeneo mengine kote nchini kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya kitaifa ya viwanda vidogo (SIDO) yatakayoanza Oktoba 23 mpaka 28 mwaka huu katika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani humo. Mtaka amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, maonyesho haya yatafunguliwa rasmi Jumanne, Oktoba 23, 2018 na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Katika maonyesho hayo, baadhi ya washiriki ni wajasiriamali na waonyeshaji wa teknolojia mbalimbali ambapo Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa ni fursa kwa wakazi wa Simiyu na maeneo ya jirani kuona ushindani katika uongezaji thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.

“Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu kujitokeza kushiriki maonyesho haya maana hii ni fursa kwao ya kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali watapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi”. Ameeleza Mtaka.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji wa SIDO Shoma Kibende amesema hadi sasa, tayari wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali wamethibitisha kushiriki  maonyesho hayo na baadhi yao wameshawasili mkoani humo.

“Wajasiriamali zaidi ya 1000 kutoka mikoa yote nchini wanatarajia kushiriki maonyesho haya na baadhi yao wameshaanza kuwasili, lakini pia kuna taasisi mbalimbali ambazo ni taasisi shirikishi na SIDO, huduma za kupata ubora hii ni fursa pekee kwa watanzania”. Amesema Kibende.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter