Home BIASHARA Tasaf yazipiga jeki kaya masikini

Tasaf yazipiga jeki kaya masikini

0 comment 36 views

Mfuko wa maendeleo ya jamii (Tasaf) wilayani longido umetoa msaada wa mizinga ya nyuki kwa kaya masikini katika kijiji cha kitendeni,tarafa ya Enduimet wilayani Longido.

Katika msaada uliotolewa mbele ya katibu tawala wa wilaya ya longido imejumisha mizinga 116 ya kufugia nyuki yenye thamani ya shilingi milioni 26 ambayo ilitolewa kwa kaya masikini 75.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo kwa kaya hizo,katibu huyo tawala alitoa pongezi kwa tasaf kwa kuwajali na kutekeleza maagizo ya serikali.

Pia licha ya pongezi hizo katibu tawala huyo aliwaasa wanufaika wa msaada huo watumie kujinasua kiuchumi badala ya kufanya starehe.

“wanufaika ni wengi mno hivyo kubalini kutumia msaada huu kubadilisha maisha yenu kupitia ruzuku hizi mnazopewa,msiende kunywea pombe wala kuongeza mke”alisema.

Mizinga hiyo imekabidhiwa kwa vikundi vitano kati ya saba vilivyopo katika kijiji hicho ambavyo vipo katika mpango wa  Tasaf.Thamani ya mizinga hiyo ni shilingi milioni 26 na itagawiwa kwa watu 75 ambao wamegawanyika katika vikundi vya watu 15 ambapo kila kikundi kitapewa mizinga 15.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter